Hali ya Maendeleo ya Sekta ya Mifugo Kuanzia Mwaka 2001 hadi Mwaka 2009
/
2010
Abstract:
Tanzania ina jumla ya hekta milioni 88.6 ambazo zinafaa kwa kilimo, hii inajuimuisha hekta milioni 60 za nyanda za malisho ambazo zinafaa kwa ufugaji. Hata hivyo, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya eneo hili (sawa na hekta milioni 24) linakaliwa kwa wingi na ndorobo, hivyo kuacha asilimia 60 (sawa na hekta milioni 36) tu zinazofaa kutumika kwa ufugaji. Kulingana na taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya 2008, idadi ya mifugo inakadiriwa kufikia ng?ombe milioni 19.1, mbuzi milioni 13.6, kondoo milioni 3.6, nguruwe milioni 1.6 na kuku milioni 56. Kati ya ng?ombe hao, 605,000 ni ng?ombe wa maziwa. Vilevile, kati ya kuku hao, milioni 22 ni kuku wa kisasa ambapo milioni 8 ni kuku wa mayai na milioni 14 ni kuku wa nyama.
[ FullText ] | [ Home ]
|